Mane inasaidia kikundi chako kusimamia fedha kwa uwazi na usalama.
Mane ni mfumo wa kidigitali kwa vikundi vya akiba, mikopo, mfuko wa jamii na Upatu. Unasaidia viongozi kurekodi miamala, kuthibitisha fedha, kutoa ripoti, kutuma SMS, na kumpa mwanachama picha sahihi ya akaunti yake.
Mzunguko wa kazi ndani ya Mane
Kila hatua inaacha kumbukumbu ili kupunguza makosa na kuongeza uwajibikaji.
Faida kuu za kutumia Mane
Mane imejengwa kwa matumizi ya kila siku ya vikundi: haraka kuingiza taarifa, rahisi kufuatilia makosa, na salama kwa taarifa za fedha.
Usimamizi wa hisa na salio
Hisa, michango na salio la mwanachama vinaonekana kwa urahisi bila kutegemea madaftari pekee.
Mikopo na dhamana
Ombi la mkopo, wadhamini, marejesho na mikopo iliyo nje vinafuatiliwa kwa mpangilio.
Mfuko wa jamii
Matukio ya jamii, michango, msaada na faini zinarekodiwa na kuthibitishwa kwa uwazi.
SMS na OTP
Mfumo hutuma ujumbe wa taarifa, uthibitisho, vikumbusho na tahadhari kwa namba za wanachama.
Ripoti za PDF na ledger
Viongozi wanaweza kutoa ripoti za miradi, mwaka, ledger na historia ya fedha kwa muda mfupi.
Usalama wa taarifa
Sessions, CSRF, security headers, approval trails na ledger controls husaidia kulinda mfumo.
Imejengwa kwa kuzingatia usalama
Ufikiaji wa taarifa unazingatia majukumu ya watumiaji, miamala nyeti inapitia uthibitisho, na kumbukumbu za mfumo husaidia kufuatilia kilichofanyika.
Jinsi Mane inavyofanya kazi
Mane inaunganisha viongozi, wanachama na rekodi za fedha kwenye flow moja. Kila role ina sehemu yake ili taarifa zisichanganyike.
Onboarding
Kikundi husajiliwa, roles huwekwa, wanachama huongezwa, na activation codes hutumika kufungua akaunti.
Daily operations
Katibu au kiongozi anaingiza michango, mikopo, jamii, faini, mikutano na taarifa za miradi.
Approvals
Miamala inayohitaji uthibitisho inapita kwa maafisa kabla ya kuathiri salio rasmi la kikundi.
Reports
Baada ya data kuingia, mfumo hutoa salio, historia, PDF reports, receipts na monthly ledger.
User manual ya haraka
Huu ni mwongozo mfupi wa kuanza. Kila mtumiaji afuate sehemu inayolingana na jukumu lake ndani ya kikundi.
Mwanachama
Angalia salio, historia na taarifa ulizotumiwa na kikundi.
- Ingia kwa username na password uliyopewa.
- Fungua dashibodi kuona salio na miamala.
- Angalia notifications kwa taarifa za mikopo, jamii na faini.
- Badilisha password au fuata forgot password ukisahau.
Katibu / Viongozi
Simamia records za kikundi na maombi yanayosubiri idhini.
- Sajili wanachama na hakikisha namba zao ni sahihi.
- Rekodi hisa, mikopo, jamii, faini na mikutano.
- Kagua approval queue kabla ya kuthibitisha muamala.
- Pakua ripoti na hakiki tofauti ya salio mapema.
Mweka Hazina
Fuatilia fedha halisi mkononi na miamala inayohitaji uthibitisho.
- Thibitisha miamala baada ya kupokea fedha.
- Linganishia cash balance na records za mfumo.
- Tumia opening balances pale kikundi kinaanza kutoka manual records.
- Ripoti tofauti yoyote kabla haijawa kubwa.
Upatu / Mchezo
Simamia mzunguko wa michango na malipo ya washiriki.
- Sajili mchezo na washiriki wake.
- Weka ratiba ya mzunguko na michango.
- Fuata dashboard kuona nani amelipa na nani anafuata.
- Tuma taarifa kwa washiriki pale inapohitajika.
Super Admin
Simamia vikundi, logins, mobilizers na matangazo ya mfumo.
- Angalia vikundi vyote na hali ya matumizi.
- Unda au kagua logins za staff pale inapohitajika.
- Tuma matangazo muhimu kwa viongozi au wanachama.
- Fuatilia inbox na reports za mfumo.
Msaada na mazoea bora
Linda akaunti na hakikisha kila hatua ina uthibitisho.
- Usishare password, OTP au activation code.
- Tumia namba sahihi za simu kwa SMS na OTP.
- Usifute records bila sababu rasmi ya kikundi.
- Ripoti tatizo la salio au login mara moja kwa support.
Tayari kuanza kutumia Mane?
Ingia kama una akaunti tayari, au sajili kikundi kipya ili mfumo uanze kukusaidia kusimamia fedha, taarifa na uwajibikaji.