Mfumo salama wa vikundi vya fedha

Mane inasaidia kikundi chako kusimamia fedha kwa uwazi na usalama.

Mane ni mfumo wa kidigitali kwa vikundi vya akiba, mikopo, mfuko wa jamii na Upatu. Unasaidia viongozi kurekodi miamala, kuthibitisha fedha, kutoa ripoti, kutuma SMS, na kumpa mwanachama picha sahihi ya akaunti yake.

3 ngazi Uthibitisho wa Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina.
SMS Taarifa za miamala, OTP, na vikumbusho kwa wanachama.
Ripoti PDF/ledger/history kwa maamuzi ya kikundi.

Mzunguko wa kazi ndani ya Mane

Kila hatua inaacha kumbukumbu ili kupunguza makosa na kuongeza uwajibikaji.

1
Sajili kikundi na wanachamaWeka taarifa za kikundi, roles, namba za simu na sera za hisa.
2
Rekodi miamalaHisa, mikopo, jamii, faini, mapato na marejesho huingizwa kwenye mfumo.
3
Thibitisha kwa maafisaMiamala nyeti inapitia approval kabla haijakamilika.
4
Toa taarifa na ripotiWanachama hupata SMS, salio, historia na ripoti za kikundi.

Faida kuu za kutumia Mane

Mane imejengwa kwa matumizi ya kila siku ya vikundi: haraka kuingiza taarifa, rahisi kufuatilia makosa, na salama kwa taarifa za fedha.

Usimamizi wa hisa na salio

Hisa, michango na salio la mwanachama vinaonekana kwa urahisi bila kutegemea madaftari pekee.

Mikopo na dhamana

Ombi la mkopo, wadhamini, marejesho na mikopo iliyo nje vinafuatiliwa kwa mpangilio.

Mfuko wa jamii

Matukio ya jamii, michango, msaada na faini zinarekodiwa na kuthibitishwa kwa uwazi.

SMS na OTP

Mfumo hutuma ujumbe wa taarifa, uthibitisho, vikumbusho na tahadhari kwa namba za wanachama.

Ripoti za PDF na ledger

Viongozi wanaweza kutoa ripoti za miradi, mwaka, ledger na historia ya fedha kwa muda mfupi.

Usalama wa taarifa

Sessions, CSRF, security headers, approval trails na ledger controls husaidia kulinda mfumo.

Imejengwa kwa kuzingatia usalama

Ufikiaji wa taarifa unazingatia majukumu ya watumiaji, miamala nyeti inapitia uthibitisho, na kumbukumbu za mfumo husaidia kufuatilia kilichofanyika.

HTTPS Role access Approval trail Session protection

Jinsi Mane inavyofanya kazi

Mane inaunganisha viongozi, wanachama na rekodi za fedha kwenye flow moja. Kila role ina sehemu yake ili taarifa zisichanganyike.

Onboarding

Kikundi husajiliwa, roles huwekwa, wanachama huongezwa, na activation codes hutumika kufungua akaunti.

Daily operations

Katibu au kiongozi anaingiza michango, mikopo, jamii, faini, mikutano na taarifa za miradi.

Approvals

Miamala inayohitaji uthibitisho inapita kwa maafisa kabla ya kuathiri salio rasmi la kikundi.

Reports

Baada ya data kuingia, mfumo hutoa salio, historia, PDF reports, receipts na monthly ledger.

User manual ya haraka

Huu ni mwongozo mfupi wa kuanza. Kila mtumiaji afuate sehemu inayolingana na jukumu lake ndani ya kikundi.

Mwanachama

Angalia salio, historia na taarifa ulizotumiwa na kikundi.

  • Ingia kwa username na password uliyopewa.
  • Fungua dashibodi kuona salio na miamala.
  • Angalia notifications kwa taarifa za mikopo, jamii na faini.
  • Badilisha password au fuata forgot password ukisahau.

Katibu / Viongozi

Simamia records za kikundi na maombi yanayosubiri idhini.

  • Sajili wanachama na hakikisha namba zao ni sahihi.
  • Rekodi hisa, mikopo, jamii, faini na mikutano.
  • Kagua approval queue kabla ya kuthibitisha muamala.
  • Pakua ripoti na hakiki tofauti ya salio mapema.

Mweka Hazina

Fuatilia fedha halisi mkononi na miamala inayohitaji uthibitisho.

  • Thibitisha miamala baada ya kupokea fedha.
  • Linganishia cash balance na records za mfumo.
  • Tumia opening balances pale kikundi kinaanza kutoka manual records.
  • Ripoti tofauti yoyote kabla haijawa kubwa.

Upatu / Mchezo

Simamia mzunguko wa michango na malipo ya washiriki.

  • Sajili mchezo na washiriki wake.
  • Weka ratiba ya mzunguko na michango.
  • Fuata dashboard kuona nani amelipa na nani anafuata.
  • Tuma taarifa kwa washiriki pale inapohitajika.

Super Admin

Simamia vikundi, logins, mobilizers na matangazo ya mfumo.

  • Angalia vikundi vyote na hali ya matumizi.
  • Unda au kagua logins za staff pale inapohitajika.
  • Tuma matangazo muhimu kwa viongozi au wanachama.
  • Fuatilia inbox na reports za mfumo.

Msaada na mazoea bora

Linda akaunti na hakikisha kila hatua ina uthibitisho.

  • Usishare password, OTP au activation code.
  • Tumia namba sahihi za simu kwa SMS na OTP.
  • Usifute records bila sababu rasmi ya kikundi.
  • Ripoti tatizo la salio au login mara moja kwa support.

Tayari kuanza kutumia Mane?

Ingia kama una akaunti tayari, au sajili kikundi kipya ili mfumo uanze kukusaidia kusimamia fedha, taarifa na uwajibikaji.

Mane

Wezesha Akaunti Yako

Kwa Katibu, Mhazini, Mwenyekiti na Wanachama waliokwisha sajiliwa

Utahitaji namba yako ya simu na msimbo wa siri uliopewa na Katibu

99.9% uptime 256-bit encrypted